Header Ads

Header ADS

Mtanzania Uganda


Ni nchi nzuri kwa kuishi na kufanya biashara. Nilifanikiwa kukaa Uganda kwa miaka mitatu na nikafanikiwa kutembelea baadhi ya sehemu kama Fort Porto, Mbarara, Lubirizi, Bushenti, Mbarara, Kasese, Igunga and Kabale. Hivyo nitaandika kutokana nay ale niliyo yaona au yasikia na kupata yaishi huko.
1.       VISA: Watanzania tunaruhisiwa kuingia na kutoka Uganda pasipo uwepo wa VISA ila maranyingi ufikapo mpakani hupewa siku kulingana na shughuri inayo kupeleka huko. Kwa wanafunzi huwa na nafasi zaidi zaidi ya hapo ni uwepo wa Shirikisho la Mashariki ya Afrika.
2.       Yellow Card: Kutokana na kubadilisha hali ya hewa, Unatakiwa kuwa na Yellow Card ambazo hutolewa katika hospitali za serikali, hii ni chanjo ambayo inatambulika kimataifha na hudumu kwa miaka kumi kama sijakosea. Kwa Dar Es Salaam ni vyema ukaenda mnazi mmoja utaipata haraka na pasipo usumbufu wowote.
3.       Passport: Popote pale passport au Hati ya kusafiria ni “Document”: Muhimu sana hivyo ni vyema ukazihifadhi kwa umakini kwani vyaweza kukuingiza matatani. Na ni vyema ukawa unatembea na kitambulisho chako hususani Passport kwani lolote laweza kukukuta na kujikuta ukitakiwa onesha utambulisho wako.
4.       Burudani: Uganda inaburudani nyingi na kwa wanao ifahamu hifananisha Kampala na Los Angels –Marekani. Ni vyema ukawa makini hapa kwani unaweza kujikuta unakula mpaka nauli hakika. Pia kuna mitaa na madanguro ya madada poa ambapo napo unatakiwa kuwa makini kwani wengine hutumia dawa za usingizi na kuishia kukuibia kila kitu.
5.       Usalama: Ni jambo la kawaida kukaguliwa kila penye halaiki ya watu iwe ni kwenye ukumbi au stendi hivyo ni vyema ukawa umejiandaa kwa ukaguzi nah ii yote ni kutokana na hali inavyo badirika kwa uhalifu wa namna mbali mbali unavyo ongezeka kila kukicha.
6.       Lugha: Kinatumika kingereza ingawa baadhi wanazungumza Kiswahili na lugha zao za asili.
7.       Kwa wazazi na wanafunzi: Kama wewe ni mzazi lissome hili kwa umakini mkubwa. Wanafunzi wa sekondari wanatabia hizi: Kujihamisha shule pale wanapo penda wakifuata marafiki na unafuu wa ada ili waweze kuwa na pesa ya matumizi, wengi hujihusisha na unywaji wa pombe na starehe za usiku, wengi hupenda kuishi nje ya shule nikimaanisha kupanga mtaani.
Ufafanuzi: Uganda kuna elimu nzuri tena sana, sifa imeharibika na wazazi wengi wanazidi poteza imani juu ya kuwapeleka watoto wao kupata elimu Uganda. KOSA wafanyalo wazazi ni hili, kuto kuwa na mawasiliano na walimu au shule husika, kuto fanya risachi ya kutosha kuhusu shule umpelekayo mwanao na zaidi ni kumwamini mwanao vya kutosha kwa kumwacha asafiri peke yake kwenda na kurudi,Ulipaji wa ada, malazi njiani na mengineyo.  Wengi huishi katika vikundi na kutembea katika vikundi na kujikuta wakiishi bila kujifunza chochote kipya.
8.       Mavazi: Mabinti huvaa mavazi mbali mbali na nguo fupi huvalika sana hususani jioni.
9.       Ufugaji wa nywele kwa wanaume: Wengi hawana mtizamo mzuri katika ufugaji wa nywele kwa mwanaume namaanisha Afro pia kusuka nywele. Utasikia maneno kama Muyaye na kadharika yakitumika yenye kumaanisha mtu mbabaishaji au asiye aminika kutokana na mwonekano wan je wa haraka haraka.
10.   Siasa: Si vyema kujihusisha na mambo ya kisiasa na mamandamano kwani polisi hawana msalia mtume katika hili.
11.   Usafiri: Kunausafiri wa aina tofauti kama Boda Boda –Usafiri wa haraka na wa hatari na Dala dala ambapo wao huziita TAXI na tax za bongo kwao huitwa SPECIAL TAXI. Vituo vya daladala huitwa stage na unapo taka kumsimamisha dereva ili akushushe sema MASAO au STAGE. Kwa kawaida daladala zao hupakiza level seat na kulipa nauli moja.
12.   Vinywaji: wanavinywaji kama Butunda, Kashera, Waragi na bia za dukani. Kuwa makini na Waragi kwani kuna baadhi ni fake na zomesha sababisha madhara mengi kwa watumiaji.
13.   Sehemu za kutembelea ukiwa huko: Munyonyo-Hoteli kubwa ya kitalii ambapo mikutano mikubwa hufanyika, Gabba Beach, sehemu nzuri kwa kula samaki wakavu, Ukiwa fortporto utaona Palace ya Mfalme wa kabila la Toro, pia ni mji ambao inasemekana umejengeka vizuri, Namugongo - Sehemu walipo uwawa mashahidi wa Uganda enzi hizo na kadharika.

No comments

Powered by Blogger.