Mtanzania Kenya
Nchi nzuri kuishi ingawa hivi punde
imetikiswa kiusalama. Nirobi pako bize sana hususani kwa sisi tunao toka Dar es
salaam na Zanzibar. Sababu za mji huu na watu wake kuwa bize muda wote ni
nyingi na sinto jikita huko.
1.
VISA:
Watanzania hawatakiwi kuingia na viza nchini Kenya ingawa ukiwa airport au
mpakani uatapewa idadi za siku kutokana na sababu ya safari yako.
2.
Pesa:
Hela inayo tumika ni Kenya Shillings na kiasi inautofauti mkubwa na Uganda na
Tanzania hasa kwenye upande wa idadi ya namba na wengu huwa tunajikuta tunapata
shida katika kuichenji au matumizi kwa ujumla. Hivyo ni vyema kila unacho nunua
jaribu kubadiri pesa inayo hitajika kwa
pesa ya Tanzania na linganisha bei ya kitu na ukiwa nyumbani Tanzania ktu hicho
hicho kinauzwa kwa bei gani.
3.
Chakula:
kama unatoka Dar es Salaam utapata tabu kidogo hasa namna chai inavyo pewa
kipaumbele. Kenya wati wanakunywa chai muda wote haijalishi ni asubuhi au sa
saba mchana nah ii inasababishwa na baridi lakini pia vitafunwa kama chapatti
na maandazi ni vingi. Wanapenda kula ugali na Chapa Jogoo ndo mpango mzima.
4.
Lugha:
Kingereza na Kiswahili hutumika ingawa wanalugha zao za asili ambazo pia
zinanguvu. Kiswahili chao kinaitwa Sheng ambapo maneno yao yanakuwa ni tofauti
kidogo namaneno ya Kiswahili. Mfano Jumamosi ni neno refu kwao ni sawa na
Saturday pia ni refu hivyo sheng huita siku hiyo Satoo, wakati Mathew anaitwa
Matoo, pia kuna maneno kama Buda, ngoma, Msee na kadharika.
5.
Mvazi: Mabinti huvaa nguo za kila aina na mabinti wa
kileo huvaa nguo fupi ambapo hivi karibuni uvaaji huu uliibua kasheshe na
kupelekea mkono wa sheria kuwaadabisha waovu waliokuwa wakiwa dharirisha
mabinti mitaani na kupelekea kufanyika kwa Kampeni ya uhuru katika mavazi,
kampeni iliyo sikika ulimwenguni kote kupitia vyombo vya habari.
6.
Siasa:
Si vyema kujihusisha na siasa ya Kenya hata kidogo. Nivyema ukawa msikilizaji
na kuishia kupambanua kichwani mwako kuliko kutaka jikita katika mambo hayo. N
kama wewe ni mwanafunzi basi usipende jihusisha pia katika siasa za vyuoni na
kujikuta ukiingia katika maandamano na kadharika, wengi wamesha poteza maisha
kwa ajiri ya ushiriki wao katika maandamano mbali mbali.
7.
Usafiri:
Wanatumia pikipiki kiasi na Daladala kwa wingi ambapo daladala zao huitwa
MaThree au Matatuu na zinatambulika kwa namba. Hivyo ni vyema mtaa unao enda
ukajua unaenda kwa namba gani na kuna utaratibu wa kupanda mabasi kwa kupanga
mstari katika baadhi ya vituo hivyo hili lisiwe jambo geni kwako. “First Come
first saved”

No comments