Mtanzania Zimbabwe
Zimbabwe ni nchi nzuri ingawa
uchumi kiasi ni Tatizo. Yanayo andikwa kwenye vyombo vya habari hususani vyombo
vya kimataifa na kufanya hata vile vya ndani kuandika kwa kuzingatia yanayo
andikwa na kusemwa na vyombo vya magharibi mengi hayana ukweli sana.
1. Tahadhari
ukiwa zimbabwe: Uzoefu nilio upata kwa siku chache nilizo kaa Zimbabwe ni huu.
Usipende kutembea tembea katika maeneo karibu na makazi ya raisi Mugabe, kama
ni mtembea kwa miguu usipite maeneo hayo wakati wa giza na kwa mchana usipite
upande barabara ilipo Ikulu yenye kumaanisha pita upande wa pili wa barabara.
Usitumie kamera
maeneo hayo hasa kwa vitu kama kuji – Selfie au kupiga picha au video
recording, Usipige makelele maeneo hayo.
2. Matumizi
ya pesa: Wanatumia dola kama pesa ya matumizi, kutokana na mzunguko wao dola
ndogo ndogo zinachafuka sana. Hivyo unapo toka Zimbabwe hakikisha umepata dola
safi kwani baadhi ya nchi huzikataa. Mfano nikiwa na dola nilizo zipata
Zimbabwe iliniwia vigumu sana kubadirisha nikiwa Afrika Kusini mpaka ikanibidi
nibadirishe kwa watu mtaani amnbapo ilikuwa ni hasara kubwa. Hili ni angalizo
ingawa si la lazima sana.
3. Lugha:
Wazimbabwe wanalugha zao ila wanatumia kingereza kama lugha ya mawasiliano na
wako – Polite pale uhitajipo msaada.
4. VISA:
Mtanzania anaruhusiwa kwenda Zimbabwe bila VISA na unaweza kuishi kwa miezi
mitatu hii ni kwa mujibu wa makubaliano ya serikali yetu na yao hivyo hili
laweza badirika muda wowote na saa yoyote, ni wajibu wako wewe kama mtanzania
kuwasiliana na balozi zetu zahuko ili kuweza jua kama kuna mabadiriko katika
hilo.
5. Ubalozi:
Ni vyema ukiwa Zimbabwe ufanye mawasiliano na ubalozi wetu kwani kunanyakati
inasaidia sana hasa pale unapo pata dharura na hakuna mtu wa kumgeukia.
6. Usafiri:
Sijajua kama imebadilika ila na wao wana daladala kama sisi na wanaziita COMBI
kama sijakosea na wakati sisi twaziita daladala. Ukiwa airport kwamfano unaweza
angukia mikononi mwa walaghai wa mjini ambao wapo kila kona hivyo ni vyema
kufanya mawasiliano na wenyeji wako mapema na kujua kiasi cha kulipa au
kuwasiliana na hoteli kwa internet kabla hujaenda.
7. Burudani:
Kunakumbi nyingi za burudani ila nilifurahishwa zaidi na Book Cafee na msanii
aliye nifurahisha ni Amara Brown na pia Vela the Plug.
No comments