Header Ads

Header ADS

Uwe ndani au nje ya Tanzania: Nini umejifunza katika ZARI All white Party?

Ni siku chache zimepita tangu mwanadada kutoka nchini Uganda ambaye kwasasa wengi tunamfahamu kwa jina la utani kama - Shemeji au wifi wa taifa afanye yake katika ulimwengu wa burudani na kukonga nyoyo za walio hudhuri. Hakika ni party ambayo inapaswa kuwa mfano wa kuigwa hasa katika swala zima la maandalizi, matangazo na kadharika.
SWALI: Tumejifunza nini kutoka kwa mjasiriamali huyu? Binafsi navutiwa na wanamaendeleo wa namna hii haijalishi ametokea wapi au anahistoria gani. MWENZANGU JE? kwenye ukweli tuseme. Mdada na wote walio husika katika maandalizi ya pati hii wameweza, na nauhakika wamevuta mkwanja mrefu haswa kutokana na event hii. ANGALIZO: Mengi yanaweza tokea hasa pesa inapo husika, hivyo kuanzia na Dangote mwenyewe na mpendwa wake hawana budi kuwa makini ili waendelee kuwa pamoja na kufanya mengi zaidi ya maana ndani na nje ya TANZANIA. Sina data kamili ya pesa walizo vuna, ila kiukweli wamevuna. HONGERA KWAO.

No comments

Powered by Blogger.