Hasara iletwayo ni BIASHARA ZA NETWORKING. Mfano FOREVER LIVING, TIENS, EDMARK, GNLD Na nyinginezo.

Kibaya zaidi ni watu wanao toa elimu ya dawa hizi.
MOJA: Wamekaa kibiashara zaidi, asikudanganye mtu, watakuja na maneno kama tunajali afya yako na kadharika , ila ukweli ni huu... Wanacheza na Afya yako. muulize kiwango chake cha elimu, utaambiwa form two au form four na nikasomea Certificate ya Business administration. SWALI la kujiuliza: UMEONA kataja amesomea Medicine au afya ya mwanadamu? Ila akianza kukuhubiria kuhusu product zake utadhani ana PHD ya Baiolojia ya viumbe hai na viungo vyake hususani mwanadamu.
Viingilio vyao: hapa pametofautiana, kuna makampuni yale ambayo yanachaji hela kubwa na yale yanayo hemea shingoni huchaji hela ndogo. Kinachotokea hapa ni hiki. wengi huingia mara baada ya kuhudhuria semina zao na kunogewa na maisha wanayo shuhudiwa kwamba nilikuwa meneja benki nikaacha na sasa nipo EDMAK, ninanyumba mbili, magari sita, ukiskia hivi nawe watamani. ulikuwa wapi miaka ya nyuma na kuwekeza pesa za mshahara wako katika vitu vinavyo dumu? Wengi tunashindwa kutofautisha kati ya ASSET na Liability. na hapa ndipo tatizo linapo kuja. Basi wakisha toa viingilio, hununua produkts kadhaa na hujaribu kuingiza wawili watatu, na mambo yakiwa magumu huacha na kurukia mtandao mwingine mpya. hiko nako hutoa kiingilio na kufanya yale yale. Usha wahi umepoteza shilingi kapi kama hivyo viingilio? hatukatai kujaribu kupo ili ufanikiwe ila hatuna buni kutumia mbongo zetu tunapo amua kujaribu.
KAMA WEWE UMEMALIZA CHUO KIKUU NA UNAFANI NA TENA HAUNA KAZI, Sikushangai. ila ukishindwa kufikiria mbinu nyingine za kujiajiri na badala yake ukaingia kwenye hizi biashara (Kumbuka umeingia huku baada ya kuwa fastreted na ushawishi na sio nafsi yako) basi nakupa ushauri wa - Kamwone daktari au mwanasaikolojia. Nakaribisha maoni na mitazamo yoyote, Lugha ni ruksa kutumia yoyote hata matusi ila kumbuka sheria isije kukubana, ukaishia kuwa victim.
No comments